MADRID, Hispania
LIONEL Messi ameshinda Tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Dunia ya ‘Goal 50’ inayotolewa na tovuti maarufu ya soka
duniani ya goal.com baada ya kumaliza msimu mwingine huku akiandika rekodi mpya.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa
Argentina alitwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu baada ya kuandika rekodi ya mabao
katika msimu ambao alivunja rekodi ya Gerd Muller iliyodumu kwa miaka 40 ya
kufunga magoli 85 katika mwaka wa kalenda.
Messi mwenye miaka 26, alifunga magoli
91 mwaka wa 2012 na kuongeza jumla ya mabao yake akiwa ndiye mfungaji kinara
mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya Barcelona baada ya kufikisha magoli
313 katika michuano yote kufikia mwisho wa msimu uliopita.
Messi alifunga katika mechi ya 19
mfululizo kwenye mechi za La Liga, Ligi Kuu ya Hispania Machi 2013, hivyo kuwa
mwanasoka wa kwanza katika historia kufunga mfululizo dhidi ya wapinzani wao
wote katika ligi kuu ya soka la kulipwa.
Baada ya kupokea tuzo yake kutoka kwa
mwakilishi wa Goal mjini Barcelona, Pilar Suarez, wakiwa kwenye uwanja wa
mazoezi wa timu hiyo, Messi alisema: "Nimevutiwa sana na tuzo. Kama
wachezaji, tunafanya kazi mwaka mzima ili kutwaa mataji kwa ajili ya timu,
hatutafuti tuzo binafsi, lakini wakati zinapokuja huwa zinatutia moyo na
kutuongezea nguvu ya kuendeleza kiwango."
Tuzo ya ‘Goal 50’ inachukuliwa kuwa
moja ya tuzo zinazoheshimiwa sana katika michezo kwa sababu uteuzi wake
hufanywa na tovuti kubwa zaidi ya soka duniani.
Kura hupigwa mwishoni mwa msimu wa
ligi za nyumbani za nchi nyingi duniani na pia wa mechi za kimataifa.
Zaidi ya waandishi 500 wa tovuti ya
Goal kutoka maeneo mbalimbali duniani hupiga kura kuchagua nyota 50-bora, hivyo
kutoa nafasi kwa wachezaji wengi zaidi.
Messi ameibuka kinara wa orodha ya
mwaka huu dhidi ya Franck Ribery aliyemaliza katika nafasi ya pili baada ya
kuisaidia Bayern Munich kutwaa mataji matatu msimu uliopita likiwamo la Ligi ya
Klabu Bingwa Ulaya. Mshindi wa mwaka jana, Cristiano Ronaldo ametwaa nafasi ya
tatu.
WASHINDI WOTE TUZO ‘GOAL 50’
2008 Cristiano
Ronaldo
2009 Lionel
Messi
2010 Wesley
Sneijder
2011 Lionel
Messi
2012 Cristiano
Ronaldo
2013 Lionel
Messi
----------
No comments:
Post a Comment