Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan |
Mbunge huyo ameamua kujisalimisha ofisi za Polisi kwa lengo la kutaka jeshi hilo lifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma dhidi yake na iwapo atabainika ni kweli ni 'zungu la unga' basi sheria zichukuwe mkondo wake.
Azan alisema aliamua kwenda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam kutokana na ukweli tuhuma hizo zimemshtua mno.
"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike na hatua za kisheria zifuate juu yangu,"alisema Azan.
"Mimi sipo juu ya sheria , itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu,"alisisitiza Azan na kuongeza:
"Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao,"alinukuliwa Mbunge huyo.
Katika barua hiyo ambayo mwandishi wake hajitaji jina, wala kuwataja wafungwa wenzake kuonyesha ni kweli anawawakilisha wala kulitaja jina la mtu aliyemuingiza kwenye biashara hiyo au 'bosi' wake aliyembebesha dawa hizo kwenda nazo Hongkong, alimtaja Mbunge huyo na watu wengine kadhaa.
Hata hivyo baadhi ya watu walioiona barua hiyo yenye kurasa tano zilizotumwa nakala zake kwa vyombo vya habari wamekuwa na shaka nayo kwa vile inaacha maswali mengi ambayo yalipaswa kujibiwa na mfungwa huyo ikiwamo yeye ni nani, aliyemuingiza ni nani na bosi wake anaitwa nani ili iwe rahisi kuendana na uhalisi wa mantiki yake kwamba amejitoa mhanga kupiga vita dhidi ya dawa hizo haramu.
No comments:
Post a Comment