STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 13, 2013

Ashanti wawafuata mabingwa wa Kagame Bunjumbura


KIKOSI cha timu ya Ashanti inaatarajiwa kuondoka mjini Kigoma kesho kuelekea Burundi kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya wenyeji wao, ili kujiandaa na pambano lao la fungua dimba kati yao na Yanga.
Ashanti iliyorejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya awali kushuka mwaka 2007 itapepetana na Yanga Agosti 24 katika moja ya mechi za fungua dimba, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Timu huyo ilikimbilia Kigoma kuweka kambi na kesho itaavuka mpaka kuelekea katika mji wa Makamba kuumana na timu ya Daraja la Kwanza nchini Burundi iitwayo Makamba.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kigoma ni kwamba mechi hiyo itachezwa keshokutwa mjini humo kabla ya Ashanti United kusogea mbele hadi Bunjmbura mwishoni mwa wiki na kuvaana na Mabingwa wa Kombe la Kagame 2013, Vital'O.
Kocha wa timu hiyo Mbaraka Hassain anaamini mechi hizo zitawasaidia kuwaweka vyema kabla ya kuwavaa Yanga ambao Jumamosi itajitupa uwanja wa Taifa kupapatana na Azam katika pambano la Ngao ya Hisani litakalochezwa uwanja wa Taifa.
Azama waliokuwa Afrika Kusini kwa ajili ya kambi yao ya mazoezi na kucheza mechi nne za kirafiki na kushinda moja na kupoteza tatu, imetua leo mchana na tayari imejichimbia katika kambi yao iliyopo Chamazi, nje ya jijini tayari kuwasubiri Yanga Jumamosi.

No comments:

Post a Comment