STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 13, 2013

Kagera Sugar yamaliza ziara Uganda kwa kipigo


BAADA ya jana kuinyuka Bunawaya ya Uganda katika mechi zake za kirafiki za kimataifa za kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bar, timu ya Kagera Sugar jioni ya leo imemaliza mechi zake nchini humo kwa kucharazwa bao 1-0 na Watoza Ushuru wa URA.
Kagera itakayofungua dimba la ligi kuu Agosti 24 dhidi ya Mbeya City, jana iliitafuna Bunawaya kwa bao 1-0 ikiwa ni mechi yao ya pili baada ya ile ya awali kulazimishwa 0-0, leo ilishindwa kuendeleza ubabe kwa URA ambao waliifunga Simba na kutoka sare ya 2-2 na Yanga kabla ya kulala kwa Coastal Union ilipokuwa nchini Tanzania mwezi uliopita.
Hata hivyo kocha msaidizi wa Kagera, Mrage Kabange amesema wanashukuru mechi hizo zimewasaidia kujiweka vyema na kuwaandaa vizuri wachezaji wao kabla ya kuanza kipute cha ligi msimu mpya.
Msimu uliopita Kagara Sugar ikiwa chini ya kocha King Abdallah Kibadeni, ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya nne, ikitanguliwa na vigogo, Yanga, Azam na Simba zilizokuwa kwenye Tatu Bora.

No comments:

Post a Comment