Baadhi ya wanamuziki wa Victoria Sound, Mwinjuma Muumin na Waziri Sonyo wakiwajibika |
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii kwenye uwanja wa Mwenge, jijini Dar es Salaam ukishirikisha michezo na wanamichezo mbalimbali wa soka, kutunisha misuli, kunyanyua vitu vizito na burudani ya muziki.
Mkurugenzi wa Home Gym, Andrew Mwangomango aliiambia MICHARAZO kuwa tayarui wadhamini wameanza kujitokeza kuwapiga tafu na kwamba tayari wamepata uthibitisho kuwa Kanali Msechu ndiye atakayekuwa mgeni rasmi.
"Kanali Msechu wa Kikosi cha 501 ndiye atakayekuwa mgeni rasmi wa tamasha letu ambalo linaendelea kuandikisha wanamichezo wanaopenda kushinda siku hiyo katika michezo wa kunyanyua vitu vizito na kutunisha misuli," alisema.
Mwangomango, aliongeza kuwa baadhi ya wadhamini wameanza kujitokeza kuwapiga tafu na kuwaomba wengine wajitokeze wakati siku zikikaribia kwa ajili ya tamasha hilo litakalopambwa na bendi ya Victoria Sound.
"Bado tunahitaji wadhamini hivyo wenye kupenda kutusaidia wajitokeze kwani ni tamasha la aina yake likiwa na michezo ya kukikimbiza na kukamata kuku, kanga na sungura na soka litakalohusisha klabu za matevetani zaidi ya 20," alisema.
Kituo hicho cha Home Gym kilichopo Mwenge-Kijijini, kilianzishwa mwaka 1998 kikitoa mafunzo wa mazoezi ya viungo na michezo ya kunyanyua vitu vizito na utunishaji wa misuli.
No comments:
Post a Comment