STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 14, 2013

Serikali yaingilia kati mzozo wa Yanga na Azam Media

HATIMAYE mkutano ulioitishwa na serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kusuluhisha mgogoro wa mkataba wa mauzo ya haki za matangazo ya Television uliowashirikisha kamati ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, klabu ya Yanga na Azam Media umemalizika hivi punde huku maamuzi kadhaa yakifikiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha mtandao huu, klabu ya Yanga ni kama imeibuka kidedea kwenye madai yake ya kupinga utaratibu mzima wa mkataba huo baina ya kamati ya ligi na Azam Media. 

Hii inakuja baada maamuzi ya mkutano huo kuamuru kwamba vipengele vya mkataba huo kupitiwa upya na klabu ya Yanga na Kamati ya Ligi na vile ambavyo vitaonekana kuwa na matatizo virekebishwe. 

Pia imeamuliwa kwamba Yanga SC itakaa kikao na Azam Media kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo kuhusu Azam pamoja na maslahi ya Yanga kupitia dili hilo la ununuaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za ligi uliofanywa na Azam Media.  


Shafii Dauda

No comments:

Post a Comment