STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 15, 2013

JKT Ruvu hawakamatiki, Kavumbangu, Maguri, Kipanga wawanasa akina Tegete, Mkude katika magoli

Didier Kavumbagu
USHINDI wa tatu mfululizo uliopata JKT Ruvu katika Ligi Kuu Tanzania Bara imeifanya timu hiyo izidi kuchanja mbuga ikiongoza msimamo wa ligi hiyo na kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wala kufungwa bao lolote mpaka sasa.
Ruvu inayonolewa na kipa wa zamani wa Tukuyu Stars na Yanga, Mbwana Makatta, iliitafuta Ashanti United jana kwa bao la Amos Mgisa na kuifanya ifikishe pointi 9 na magoli sita ya kufungwa huku yenyewe ikiwa na ukuta wa chuma kwa kutoruhusu kufungwa bao lolote.
Kikosi cha JKT Ruvu
Simba ambayo ilianza mechi zake kwa kulazimishwa sare ya wageni Rhino Rangers imechupa hadi nafasi ya pili kutokana na ushindi wa mechi yao ya jana dhidi ya Mtibwa Sugar, huku Ruvu Shooting ikiwa kwenye nafasi ya tatu kutokana na jana kuing'ata  Mgambo JKT.
Bao pekee lililofungwa na Elius Maguri lilitosha kuifanya maafande hao kufikisha pointi sita, huku mfungaji huyo akiingia kwenye orodha ya wafungaji watano wanaoongoza kwa sasa katika ligi hiyo kila mmoja akiwa na mabao mawili.
Maguri aliyesajiliwa na Ruvu Shooting toka Prisons ameungana na akina Jerry Tegete na Didier Kavumbagu wa Yanga, Jonas Mkude wa Simba, Saad Kipanga aliyeanza kuonyesha makeke licha ya ugeni wake katika ligi hiyo naye akiwa na mabao mawili baada ya jana kuisaidia timu yake ya Rhino kupata sare dhidi ya Olojoro JKT jijini Arusha.
Mchezaji mwingine aliye katika orodha hiyo ya wafungaji bora kwa sasa wakati ligi ikiwa ndiyo kwanza ipo raundi ya tatu ni Bakar Kombo wa JKT Ruvu.
Wakati Prisons ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijafanikiwa kufunga bao lolote mpaka sasa angalau wenyewe wameambulia pointi jana jijini Tanga mbele ya Coastal, kuliko Ashanti United ambayo licha ya kuwa na goli moja, lakini haijaonja furaha ya kumiliki pointi baada ya kupoteza mechi zake zote tatu.
Ilianza kwa kufungwa na Yanga mabao 5-1 kabla ya kunyolewa bao 1-0 katika mechi zilizofuata dhidi ya Mgambo na jana JKT Ruvu na kuwa ndiyo inayoburuza mkia ikizibeba timu zote za ligi hiyo yenye klabu 14.
Ashanti ni kati ya timu tatu zilizopanda daraja msimu huu sambamba na Rhino Rangers iliyokusanya pointi mbili mpaka sasa katika mechi zake tatu na Mbeya City iliyokaribia kuiadhiri mabingwa watetezi Yanga jana kwenye mechi yao ilioisha kwa sare ya 1-1 yenyewe ikiwa na pointi tano sambamba na klabu nyingine wakiwamo Yanga, Coastal Union na Azam.
Msimamo kamili wa ligi hiyo baada ya mechi ya jana ni kama ifuatavyo na wafungaji na ratiba ya mechi zijazo utachungulia hapo chini:

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014                                         
                                     P  W  D  L    F  A  GD PTS
1.  JKT Ruvu                 3    3   0   0   6   0    6    9
2.  Simba                       3    2   1   0   5   2    3    7
3.  Ruvu Shooting           3    2   0   1   5   2    3    6
4.  Yanga                        3    1   2   0   7   3   4    5
5.  Azam                        3    1    2   0   4   2   2    5
6.  Coastal Union            3   1    2    0   3   1  2    5
7.  Mbeya City                3   1    2    0   3   2   1   5
8.  Mtibwa Sugar             3   1    1   1    2   3  -1  4
9.  Mgambo                    3    1    0   2    1   3  -2   3
10. Rhino Rangers           3    0    2   1    3   5  -2   2
11. Kagera Sugar            3    0    2    1   1   2  -1   2
12. Oljoro                       3    0    1    2   1   4  -3   1
13. Prisons                      3    0    1    2   0   6  -6   1
14. Ashanti                      3    0    0    3   1   7  -6   0

Wafungaji:

2- Jerry Tegete, Didier Kavumbangu (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Elias Maguri (Ruvu Shooting), Saady Kipanga (Rhino Rangers)
1- Abdi Banda, Crispian Odulla, Jerry Santo (Coastal Union), Haruna Chanongo, Henry Joseph, Betram Mombeki (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva (Yanga), Iman Joel (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Khamis Mcha, Aggrey Morris (Azam), Mwagani Yeya, Steven Mazanda, Paul Nonga (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Ayoub Kitala, Jerome Lembeli (Ruvu Shooting), Juma Luzio, Masoud Ally (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Salum Machaku, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga (Mgambo JKT), Themi Felix (Kagera Sugar), Amir Omary (Oljoro JKT)

Mechi zinazofuata siku ya Jumatano 
Sept 18, 2013Prisons vs Yanga
Simba vs Mgambo JKT
Kagera Sugar vs JKT Oljoro
Azam  vs Ashanti United
Coastal Union  vs Rhino Rangers
Mtibwa Sugar  vs Mbeya City
Ruvu Shooting vs  JKT Ruvu

No comments:

Post a Comment