STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 15, 2013

Gareth Bale aanza na bao Real Madrid ikipata sare ugenini la liga

bale bale bale bale
NYOTA mpya wa Real Madrid na mchezaji ghali kuliko wote duniani, winga Gareth Bale usiku wa kuamkia leo alianza makeke yake katika klabu yake kwa kuifungia moja ya mabao yaliyoisaidia vinara hao wa Hispania wasiumbuke ugenini walipotoka sare ya 2-2 na Villareal.
Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur na alionyesha uwezo mkubwa, akifunga bao hilo la kusawazisha baada ya wenyeji kuwatangulia Madrid kwa bao la Cani na kufanya hadi mapumziko timu hizo ziwe nguvu sawa ya bao 1-1.
Kipindi cha pili Cristiano Ronaldo aliiongezea Madrid bao ambalo hata hivuo lilikuja kurejeshwa na wenyeji kupitia kwa Giovani Dos Santos.
Katika mechi iliyochezwa mapema leo, Espanol ikiwa ugenini imeizabua Granada kwa bao 1-0 lilitupiwa kambani na Lanzarote.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa jana katika ligi hiyo maarufu kama La Liga, mabingwa watetezi Barcelona ikiwa nyumbani ilishinda mabao 3-2 dhidi ya Sevilla, shukrani ya mabao ya Dani Alves , Lionel Messi na Alexis Sanchez.
Wageni mabao yao yalitupiwa kimiani na Coke na Ivan Rakitic. Nao Atletico Madrid walipata ushindi wao wa nne mfululizo kwa kuwalaza Almeria mabao 4-2 na kuwaweka kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakati Levante walilazimishwa suluhu na Real Sociaded.

No comments:

Post a Comment