STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 11, 2013

Yanga yamkana Stewart yasisitiza Brandts mwanzo mwisho

Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Young Africans umesema hauna mpango wa mazungumzo yoyote na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Azam FC muingereza Stewart Hall juu ya kumpa ajira ya kuwa kocha na Ernie Brandts bado anaendelea na kazi yake ya ukocha mkuu.

Taarifa hii ya uongozi wa klabu ya Yanga inafuatia kuzagaa kwa taarifa hizo leo mchana kwenye baadhi ya mitandao mbali mbali ya kijamii kuwa wapo katika maongoezi na kocha huyo ili achukue nafasi ya kocha mholanzi Ernie Brandts.

Msiumizwe vichwa na taarifa hizo kwani wengi wao lengo lao ni kutaka kuivuruga Yanga sasa ili isiweze kufanya vizuri katika mzunguko unaofuata na mashindano ya kimataifa, uzuri tumelijua hilo na sisi tunauambia umma hatuna mazungumzo na kocha huyo na wala hatujawahi fikiria kufanya hivyo.

Tunaomba umma wa wapenzi wa soka nchini, wanachama, washabiki na wapenzi wa Young Africans watamabue kuwa Ernie Brandts bado ni kocha mkuu wa klabu yetu na hatuna mpango wa kufanya mabadiliko na wala hatujawahi kufikiria kufanya hivyo.

Mholanzi Ernie Brandts anatarajiwa kurejea nchini jumapili Novemba 24, 2013 tayari kabisa kwa kuanza mazoezi na vijana wake siku ya jumatatu Novemba 25, 2013 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Hisani (Nani Mtani Jembe) dhidi ya Simba SC Disemba 14, 2013.

Mara baada ya mchezo huo kikosi kitaendelea na maandalizi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu pamoja na mashindano ya kimataifa lakini pia timu inategema kushiriki wa mashidano ya Mapinduzi Cup kisiwani Zanzibar mapema mwezi Januari 2014. 

Msimu wake wa kwanza ameiongoza Yanga kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na hivi sasa anaongoza msimamo wa Ligi kwa kuwa na pointi 28 na mabao 31 ya kufunga na mabao 11 ya kufungwa.

Kocha Brandts mara baada ya mchezo wa mwisho dhidi ya JKT Oljoro alitoa mapumziko ya wiki mbili kwa wachezaji wake na benchi la ufundi kwa ajili ya kuwa na familia zao na mapumziko na ambapo timu inatarajiwa kuanza tena mazoezi tarehe 25 Novemba kujiandaa na michezo itakayokuwa inawaikabili timu. 


YSC

No comments:

Post a Comment