STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 11, 2013

Said Mbelwa, Karama Nyilawila washinda kwa KO

Bondia Said Uwezo (kushoto) akipambana na Sindano Paul  wakati wa mchezo wao uliofanyika jumapili katika ukumbi wa Zulu Paradise, Pugu Kilumba Dar es Salaam uwezo alishinda kwa pointi mpambano huo.
Refarii Saidi Chaku katikati akimnyosha mkono juu bondia Said Uwezo baada ya kumshinda kwa point mpinzani wake

Mabondia Kaminja Ramadhani (kushoto) na Karama Nyilawila wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili. Karama alishinda kwa KO ya raundi ya kwanza.

Bondia Twalibu Mchanjo (kushoto) akipambana na Mohamed Kashinde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili. Mchanjo alishinda kwa KO ya raundi ya tatu katika mpambano huo uliokuwa wa kusisimua

Bondia Shabani Kaoneka (kushoto) akipambana na Saidi Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika jana, Mbelwa alishinda kwa KO ya raundi ya kwanza baada ya kumkalisha chini mpinzani wake kwa konde kali na kushindwa kuendelea.

Bondia Shabani Kaoneka akiwa chini hoi huku akihesabiwa na mwamuzi kulia ni mpinzani wake Said Mbelwa akimsubiri kwa hamu, hata hivyo pambano huo ulisha hapo hapo na Mbelwa kufanikiwa kushinda kwa KO ya raundi ya kwanza.

No comments:

Post a Comment