STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 25, 2013

Msondo, Sikinde kumaliza ubishi leo TCC-Chang'ombe

Safu ya uimbaji wa Sikinde
Msondo Ngoma wakionyesha makeke yao

MABINGWA na wakongwe wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' na Mlimani Park Orchestra 'Wana Sikinde' leo mchana watachuana vikali katika viwanja vya TCC Club  Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo wa kusherekea sikukuu ya Krismasi utakuwa wa kufunga mwaka 2013 na pia utaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wa muziki wa dansi nchini mwaka huu.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema mpambano huo utaanza saa nane alasiri hadi majogoo.
Kapinga alisema Sikinde wataingia TCC wakitokea Bagamoyo walipokuwa wakipiga kambi wakati kambi ya Msondo Ngoma imebaki kuwa siri kwa muda wote.
Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa shaka ya hujuma.
Kapinga alisema kila bendi itatapewa muda wa saa moja kupiga jukwaani kabla ya kuipisha nyingine.
Kiongozi wa Msondo Ngoma, Saidi Mabera alisema jana kuwa watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaibuka kidedea.
Alitaja baadhi ya nyimbo watakazopiga kuwa ni  'Nimuokoe Nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali' na  'Suluhu'.
Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.
“Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.
Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Selina', Wikiendi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi’, 'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.
Pambano limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, gazeti la NIPASHE, CXC Africa na tovuti ya Saluti5.com.

No comments:

Post a Comment