STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 25, 2013

Mtawala amshafisha Rage fedha za Okwi


Mtawala (kushoto) akiteta jambo na Rage

Emmanuel Okwi
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Klabu ya Simba, Evodius Mtawala, amesema amefurahi kuiacha klabu hiyo ikiwa na rekodi nzuri ya kumfunga mtani wake Yanga mabao 3-1 na kuweka wazi kwamba mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage, hajatafuna fedha za usajili wa mshambuliaji wao wa zamani, Emmanuel Okwi.
Mtawala jana alitangazwa rasmi kuwa Mkurugenzi mpya wa Vyama, Wanachama na Masuala ya Kisheria wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Hata hivyo, Mtawala aliweka wazi kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Hanspoppe Zacharia, ndiye mtu anayeidai klabu hiyo kiasi kikubwa cha fedha.
Mtawala alisema yeye na Hanspoppe walikwenda Tunisia kukutana na viongozi wa Klabu ya Etoile du Sahel kuzungumzia malipo ya Dola za Marekani 300,000 za mauzo ya Okwi na hakuna mahali walipoonyesha kwamba kuna kiasi cha fedha walilipwa.
"Kuhusiana na fedha za Okwi, hazijaliwa, hilo hata mimi namtetea," alisema Mtawala.
Kiongozi huyo mpya wa TFF anayeshika nafasi ya Mtemi Ramadhani, alisema katika kipindi cha uongozi wake alijitahidi kulipa madeni mbalimbali yaliyokuwa yanawakabili ili kuendeleza uhusiano mzuri na taasisi walizokuwa wanafanya nazo kazi.
Alisema amefurahi kuona anaiacha Simba ikiwa na rekodi mbili nzuri za kuwafunga Yanga na kuendelea kuwaumiza vichwa viongozi, wanachama na mashabiki wao.
Aliweka wazi kuwa hakutaka kujihusisha na mgogoro wa uongozi ndani ya Simba na alihakikisha timu inaandaliwa vyema ili kupata matokeo mazuri.
"Watanikumbuka, kuna mambo mengi nilikuwa ninamshauri mwenyekiti (Rage) na wajumbe, kama wangenisikiliza, huu mvutano uliopo sasa usingekuwepo," alisema Mtawala.
Alifafanua kuwa, akiwa TFF atahakikisha anatekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu na muongozo kama ilivyoelezwa kwenye katiba ya shirikisho hilo.
Alisema yuko tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye nafasi hiyo mpya na anaahidi kuwa mwadilifu na kufuata misingi ya kazi hiyo.
Mtawala ambaye kitaaluma ni mwanasheria, aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu Simba jana Desemba 24.

NIPASHE

No comments:

Post a Comment