STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 25, 2013

Breaking News: James Kisaka is no more

James Kisaka enzi za uhai wake
HABARI zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kuwa aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Jamse Kisaka amefariki dunia.
Kisaka aliyewahi kung'ara katika nafasi ya ukipa ndani ya Simba na klabu nyingine alikuwa amelazwa hospitali wiki kadhaa sasa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza na kutoona na aliakuwa akiendelea kuimariksa.
MICHARAZO inaendelea kufuatilia tarataibu za mazishi za kipa huyo nyota wa zamani na kocha aliyejizolea sifa kemkem za ufanisi wa kazi yake.
James Kisaka alizaliwa mwaka 1955 mjini Dar es Salaam na alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya Oysterbay na baadaye sekondari za Mzizima na Tambaza, Dar es Salaam pia.

Alianza kupata umaarufu wa soka tangu anasoma na haikushangaza aliposajiliwa na Sigara akiwa nba umri mdogo.

Baadaye alichezea Nyota Nyekundu, Simba kabla ya kwenda Small Simba ya Zanzibar na baadaye Volcano ya Kenya alipokwenda pamoja na Zamoyoni Mogella na Lilla Shomari na kisha kutua Ndovu ya Arusha.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Simba kilichokwenda ziara ya mafunzo nchini Brazil mwaka 1981.
Kisaka atakumbukwa kwa upole wake na ufanyaji kazi kwa bidii enzi za uhai wake. 
Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema. Ameen

.

No comments:

Post a Comment