STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 2, 2014

Simba yaidonyoa Leopards kimoja Mapinduzi Cup

Haruna Shamte akimtoka mchezaji wa AFC Leopards

Kikosi cha Simba kilichoshinda jana
Leopards waliopigwa kimoja na Simba (Picha zote:ZanziNews)
 KLABU ya Simba bila ya kocha wake mkuu., Mcroatia Zdavko Logarusic usiku wa jana iliwapa raha mashabiki wake baada ya kuwatungua AFC Leopards ya Kenya kwa bao 1-0 katika mfululizo wa michuano yta Kombe la Mapinduzi iliyoanza jana visiwani Zanzibar.
Bao pekee la Simba liliwekwa kimiani na kiungo nyota, Amri Kiemba aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Awadh Juma 'Maniche' katika dakika ya 77 na kuipa Simba ushindi huo ikiwa chini ya kocha msaidizi, Suleiman Matola.
Michuano hiyo inayoshirikisha timu 12 inatarajiwa kuendelea jioni ya leo kwenye viwanja viwili vilivyopo Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment