STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 6, 2014

48 wanaswa vurugu za Morogoro


  Wakazi wa doma wilayani Mvomero wakiwa mbaroni kwa tuhuma za kufunga barabara ya Morogoro na Iringa wakishinikiza wafugaji kuondolewa eneo hilo.
WATU 48 wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufunga barabara ya Morogoro na Iringa wakishinikiza wafugaji wa jamii ya Kimasai kuhamisha katika eneo la Doma wilayani Mvomero.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Februari 6 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi.
Kamanda huyo alisema kuwa katika tukio hilo walifanikiwa kuwatia mbaroni wanawake 24 na wanaume 24 ambao wanadaiwa kufanya vurugu hizo.
Alisema kuwa fujo hizo zilitokea baada ya watu hao kudai kuwa wafugaji hao waliwapiga na fimbo wananchi wenzao waliokwenda porini kukata mkaa jambo lililowafanya nao kuamua kufunga barabara hiyo.
Hata hivyo kamanda huyo alisema kuwa walifanikiwa kufungua barabara hiyo majira ya saa 7 mchana baada ya kupiga mabomu ya mchozi kwa lengo la kuwatawanya wananchi hao.
Alisema kuwa hakuna madhara yeyote ya kibinadamu yaliotokea ingawa watu hao walijaribu kuwapiga mawe polisi hao .
Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kwamba watu hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho ili kuweza kujibu tuhuma hizo.
Kwa upande wao wananchi hao wamalalamikia wafugaji hao kitendo chao cha kuingiza mifugo mashambani na kuharibu mazao njambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.
Pia walilalamikia uongozi wa kijiji hicho cha Doma kwa kuwaingiza wafugaji kinyemela hali inayofanya kuwa wengi huku eneo la malisho likiwa dogo hali inayofanya wafugaji hao kuingiza mifugo yao mashambani.
Ibrahim Ndegalo alisema kuwa mbali na wafugaji hao kuwapiga lakini pia wamakuwa wakiwanyang’anya mali zao bila sabababu na kwamba maisha yao yamekuwa hayana amani.
 Credit:MACHAKU

No comments:

Post a Comment