STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 6, 2014

Mchungaji afa maji akiiga kutembea juu ya maji kama YESU

KUTEMBEA juu ya maji siyo kazi rahisi na pengine inaweza kugeuka kilio kama mtu huna imani ya kutosha. 
Huko Nigeria mwanzoni mwa mwezi uliopita ilikuwa sikitisho kubwa kwa waumini baada ya mchungaji wao kusombwa na maji baada ya kujaribu kutembea juu ya maji kama vile Nabii Yesu alivyofanya wakati wake alipokuwa duniani.

Pastor Frank Kabele mwenye umri wa miaka 35, aliwaambia waumini wake kuwa mtu mwenye imani anaweza kufanya miujiza yeyote ila tu uwe na imani. 
Aliwaahidi wafuasi wake kuwa atatembea juu ya maji pindi tu atakapomaliza maombi yake. 
Lakini mambo yalienda ndivyo sivyo baada ya pastor huyo kujaribu kutembea katika mto mkubwa, alididimia mtoni humo na ilikuwa vigumu kwa waumini wake kumsaidia kwani maji yalikuwa na nguvu nyingi.
chanzo-http://www.zimeye.org/

No comments:

Post a Comment