STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 21, 2014

Al Ahly yaitumia salamu Yanga ikitwaa Super Cup

 USHINDI iliyopata Al Ahly ya kunyakua taji jingine la Super Cup dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia ni kama salamu kwa mabingwa wa soka nchini, Yanga watakaovaana nao kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Majabali hao wa Afrika kutokea Misri waliishindilia warabu wenzao kwa mabao 3-2 katika mechi ya fainali iliyochezwa usiku wa jana na kuhudhuriwa na kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface aliyeenda kuifanyia ushushushu  kabla ya kuvaana nao wiki ijayo.
Watetezi hao wa Ligi hiyo ya Mabingwa Afrika walipata ushindi wao kupitia mabao Gedo aliyefunga katika dakiia ya23  kabla ya  Amr Gamal aliyefunga mawili dakika ya 54 na 69.
Mabao ya wapinzani wao ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika yaliwekwa kimiani na Maaloul dakika ya 63 na Ben Youssef dakika ya 78.
Huenda Mkwasa amepata somo zuri na salama atakazowafikishia vijana wake kwamba wanapaswa kucheza namna gani ili kuhimili bishindo vya timu hiyo iliyotwaa taji la Afrika mara nane na kuweka rekodi.

No comments:

Post a Comment