STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 21, 2014

Spurs wafa ugenini, Juve, Valencia zikitakata Ueropa League

 

WAKATI Tottenham Hotspur ikilazwa ugenini na timu ya Dnipro ya Ukraine, Juventus wameifumua Trabzonspor kwa mabao 2-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga 16 Bora ya Ligi Ndogo ya Ulaya (Europa League).
Spurs ambayo ilipoteza mkwaju wa penati uliopigwa na nahodha wake Michael Dawson ambao huenda ungewasaidia kupata sare ugenini na kuwa na kazi nyepesi kwenye mechi ya marudiano dhidi ya wapinzani wao, walifungwa bao hilo la pekee kwenye dakika ya 81 kwa mkwaju wa penati.
Penati hiyo ilitumbukizwa kimiani na Yevhen Konoplyanka na kuifanya Spurs kuwa na kazi ya kuhakikisha wanashinda mechi ya nyumbani wiki ijayo kama inataka kufuzu 16 Bora.
Katika mechi nyingine, mabingwa wa Italia waliotupwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, Juventus iliifumua Tarbzonspor kwa mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa mjini Turin, Italia.
Mabao ya Dani Osvaldo la dakika ya 15 na jingine la lala salama ya mchezo huo kupitia kwa Paul Pogba yaliipa uhakika Juve kuwa na kazi nyepesi kwenye mechi ya marudiano ugenini wiki ijayo.
Nayo timu ya Lazio ya Italia walipata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ludogorets ya Bulgaria, huku Eintracht Frankfurt  ya Ujerumani ikitoka nyuma kwa mabao mawili na kupata sare ya 2-2 dhidi ya Porto ya Ureno.
Mabao ya Ricardo Quaresma na Silvestre Varela ya kila kipindi yaliipa uongozi Porto kabla Joselu  kufunga bao moja na Alex Sandro kuisaidia wageni toka Ujerumani kwa kujifunga dakika ya 78.
Fiorentina ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Esbjerg, Sevilla ikitoka sare ya 2-2 na Maribor nayo Shakhtar Donetsk ikipata sare ya 1-1 dhidi ya Viktoria Plzen, huku Rubin Kazan waliocheza pungufu  ya mchezaji mmoja ugenini iliambulia sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji wa Real Betis. Wageni walimpoteza nyota wao Alexander Prudnikov aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 28.
Benfica ilishinda 1-0 dhidi ya PAOK Salonika, huku  AZ Alkmaar ikishinda kama hivyo mbele ya Slovan Liberec, nazo timu za  Chornomorets na Lyon, Anzhi Makhachkala na Genk zikitoka suluhu ya kutofungana katika mechi zao mbili tofauti huku Valencia wenyewe walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Dynamo Kiev.

No comments:

Post a Comment