STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 19, 2014

Barcelona, PSG zaua ugenini Ligi ya Mabingwa Ulaya


Messi akifunga penati iliyolalamikiwa na kocha  Pellegrini
Ibrahimovic akifunga moja ya mabao yake, chini akishangilia bao lake la kwanza

Add caption
KIPIGO cha kustukiza cha mabao 2-0 walichopewa Manchester City ikiwa nyumbani kwao na Barcelona kimemtibua kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini kumtupia lawama refa wa pambano hilo la awali la mtoano kuwania kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akidai aliwabeba na kuwatengenezea ushindi wapinzani wao.
Pellegrini anailalamikia penati iliyotolewa kwa wapinzani  iliyosababishwa na kufungwa na Lionel Messi dakika tisa baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Messi aliangushwa nje kidogo na eneo la penati na Martin Demichelis na refa Jonas Eriksson kuamuru ipigwe adhabu hiyo na Messi kuifungia Barcelona bao la kuongoza kabla ya beki Dani Alves kuongeza la pili dakika ya 90 na kuiweka Barca katika nafasi nzuri ya kutinga robo watakapoikaribisha Manchester City kwenye mechi ya marudiano Machi 11.
Pellegrini amenukuliwa akisema anashangaa ni vipi UEFA hata ikamteua mwamuzi huyo kutoka Sweden kuchezesha pambano kubwa kama hilo, huku akidai mara kadhaa amekuwa wakiionea timu yake.
Hata hivyo matamshi hayo ya kocha huyo kutoka Chile yanaweza kumweka matatani kwa 'mabosi' wa UEFA.
Katia mechi nyingine ya michuano hiyo hatua ya 16 Bora, mabingwa wa Ufaransa, PSG ikiongozwa na Zlatan Ibrahimovic, iliisasambua Bayer Liverkusen nyumbani kwao kwa kuichabanga mabao 4-0.
Wanafainali hao wa michuano ya mwaka jana wakiwa kwenye uwanja wao wa BayArena mjini Leverkusen, nchini Ujerumani walishindwa kuamini kipigo walichopewa na Wafaransa hao ambao ni kama wamejihakikishia hatua ya robo fainali kwa vile Leverkusen watalazimika kuifunga PSG mabao 5-0 jijini Paris ili kuiondosha kitu kinachoonekana kuwa kigumu, japo soka lolote linaweza kutokea.
Mabao ya wababe hao wa Ufaransa yalifungwa na Blaise Matuidi dakika ya tatu kwa pasi ya Verratti, kabla ya Ibrahimovic kuongeza la pili dakika ya 39 kwa mkwaju wa penati na kisha kufunga jingine dakika 42 akimaliza pasi Matuidi.
Bao la nne lililoikata maini Wajerumani nyumbani kwao liliwekwa kimiani na mchezaji mpya wa timu hiyo kutoka Newcastle United, Yohan Cabaye aliyefunga katika dakika ya 88 akimaliza pasi ya Lucas.

No comments:

Post a Comment