STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 19, 2014

Breaking News! Ajali yaua wanne Sekenke

Wananchi wakiangalia Lori baada ya kuteketea kwa moto baada ya kuporomoka korongoni
 Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii
 Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

 Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
 Hii ni njia ya mlima sekenke

AJALI mbaya imetokea jioni hii baada ya Lori la Mafuta kuanguka na kuteketea katika eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo. Shuhda wa ajali hiyo bwana Julius chacha alipoongea na mtandao wetu wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto. Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment