Na Mwandishi Wetu, Mbeya
JUMLA ya wachezaji 16 wa kikosi cha
Maboresho ya Timu ya Taifa(Taifa Stars) wamechaguliwa kujiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya mechi za kirafiki kutoka kambi
ya wachezaji 34 iliyokuwa Chuo cha Ualimu Tukuyu Wilaya ya Rungwe
mkoani Mbeya.
Kikosi hicho kimetangazwa leo na
Kocha Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na
waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo
jijini Mbeya.
Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni
Mlinda mlango Benedict Mlekwa kutoka Mara, Walinzi wa kati ni Emma Simwanda kutoka Temeke na Joram Mgeveja kutoka Iringa.
Walinzi wa pembeni ni
Omari Kindamba wa Temeke, Edward Mayunga wa Kaskazini Pemba
na Shirazy Sozigwa wa Ilala, viungo ni Yusufu Mlipili, Said Juma Ally kutoka Mjini Magharibi, Abubakar Mohamed wa Kusini Unguja na Hashimu Magona kutoka Shinyanga.
Viungo wa pembeni ni Omari Nyenje wa Mtwara na Chunga Zito
kutoka Manyara.
Washambuliaji ni Mohammed Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu Lipati wa Ilala,
Abdurahman Othman kutoka Mjini Magharibi na Paul Bundara kutoka
Ilala.
Aliongeza, katika kikosi hicho pia
wamejumuishwa wachezaji wawili waliojiunga na Timu ya Taifa ya vijana U20; Mbwana Mshindo kutoka Tanga na Bayaga Fabian
kutoka Mbeya.
Manyanga alisema wachezaji
wengine walioachwa wataendelea kuwa kwenye uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu(TFF) kwa sababu mpango wa maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu.
Alisema Kambi ya timu hiyo iliyoanza Machi
22, imehitimishwa leo Aprili 17 kwa awamu ya kwanza ambapo
wachezaji hao watajiunga na kikosi cha Stars mechi ya Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya
Kambi ya awamu ya Pili.
No comments:
Post a Comment