STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 28, 2014

Barca chupuchupu, Messi aibeba yaiengua Real Madrid

http://e2.365dm.com/14/04/660x350/Lionel-Messi-Barcelona-2014_3132310.jpg?20140427222759
http://peruzonatv.com/wp-content/uploads/2014/03/Barcelona-vs-Osasuna-en-vivo.jpg?0e806a
Messi akishangilia bao lake na wachezaji wenzake wa Barcelona
KLABU ya Barcelona usiku wa kuamkia leo imeponea tundu la sindano baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Villarreal na kuzidi kuendelea kuwepo kwenye mbio za ubingwa.
Bao la dakika ya 83 kupitia kwa Lionel Messi akimalizia kazi nzuri ya Cesc Fabregas na mawili ya kujifunga ya wachezaji ya Villarreal ndiyo yaliyoibeba Barca waliotanguliwa kufungwa na wenyeji wao.
Cani aliifungia Villarreal bao la kuongoza dakika ya 45 akimalizia kazi nzuri ya Jonathan Pereira kabla ya Trigueros kuongeza la pili dakika ya 55 baada ya kumegewa pande na Aquino.
Hata hivyo mabao mawili ya kujifunga kupitia kwa Gabriel Paulista dakika ya 65 na jingine la dakika ya 78 kupitia kwa Musacchio yalifanya matokeo kuwa mabao 2-2 kabla ya Messi kufunga bao la ushindi dakika ya 83 na kuwapa Barca ushindi huo muhimu.
Matokeo hayo yameifanya Barca kufikisha jumla ya pointi 84 na kuchupa toka nafasi ya tatu hadi ya pili wakiishusha Real Madrid yenye pointi 82, na pointi nne nyuma ya vinara Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment