STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 28, 2014

Suarez ndiye Mwanasoka Bora England


MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool, Luis Suarez ambaye jana alishindwa kuinusuru timu yake kuepuka kipigo toka kwa Chelsea ameteuliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka.
Eden Hazard wa Chelsea alishika nafasi ya pili katika tuzo hiyo ya wachezaji wa kulipwa PFA Player of the Year na kiungo wa Manchester City, Yaya Toure alinyakua nafasi ya tatu.
Suarez ambaye anakumbukwa kwa vituko alivyofanya kwa msimu uliopita anakuwa mchezaji wa pili wa Liverpool kunyakua tuzo hiyo katika miaka 25 iliyopita baada ya nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard kufanya hivyo mwaka 2006. Klabu hiyo ilishawahi kunyakua tuzo hizo nne kati ya mwaka 1980-88 kupitia wachezaji wake wa zamani Terry McDermott, Kenny Dalglish, Ian Rush na John Barnes.
Suarez kufikia mafanaikio hayo baada ya kuifungia timu yake mabao 30 na ndiye anayeongoza matumaini ya timu yake kukatisha ukame wa miaka 24 ya kunyakua taji la Ligi Kuu ya England.Kabla ya kutwaa tuzo hiyo, Suarez alipamba vyombo vya habari za England na matukio aliyowahi kuyafanya siku za nyuma ikiwamo kumng'ata beki wa Chelsea  Chelsea Branislav Ivanovic na lile tukio la kudaiwa kumfanyia ubaguzi nahodha wa Manchester United, Patrick Evra na kutozwa faini na kusimamishwa mechi kadhaa.
Mchezaji huyo toka Uruguay pia alijumuishwa kwenye kikosi cha msimu sambamba na Eden Hazard wa Chelsea aliyetajwa kama mchezaji mchanga wa mwaka huu, Daniel Sturridge na nahodha wa Liverpool Steven Gerrard.
Wengine katika kikosi hicho ni; Kipa wa Chelsea aliye majeruhi kwa sasa Petr Cech, Gary Cahil, Yaya Toure, Vincent Kompany, Luke Shaw, Adam Lallana, Seamus Coleman wa Everton.

No comments:

Post a Comment