STRIKA
USILIKOSE
Monday, April 28, 2014
Simba yaomboleza kifo cha Muchacho, yafafanua suala la katiba
MWENYEKITI wa Simba SC, Mhe; Ismail Aden Rage, ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa, marafiki na familia ya Marehemu Abdulrahman Muchacho (66), aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam na kuzikwa juzi katika makaburi ya Kisutu jijini.
Muchacho ni miongoni mwa wanachama wenye historia ya kipekee ndani ya klabu kwani akiwa Timu Meneja wa Timu ya Simba mwaka 1976, Simba iliifunga Yanga mabao 6-0, ambao ndiyo mshindi mnono zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mechi za Watani wa Jadi na akiwa Mweka Hazina wa Timu katika miaka ya 1990, Simba ilicheza katika Fainali ya Kombe la CAF.
Mwanachama huyu ndiye pia chachu ya kuanzishwa kwa kundi la ushangiliaji la Muchacho ambalo ndilo chimbuko la makundi yote ya ushingilijiaji katika viwanja vya soka hapa nchini.
"Kwa kweli msiba huu umenigusa sana hasa ukizingatia kwamba niliona utendaji wake wakati mimi nikiwa mchezaji wa Simba na baadaye katika uongozi. Msiba wa Muchacho ni mkubwa kwa klabu kwa sababu jina lake litabaki kuwa sehemu ya historia iliyotukuka ya Simba SC.
"Muchacho anatoka katika familia ya wana Simba. Baba yake alikuwa shabiki mkubwa wa Sunderland na mrehemu alikuwa mrithi mzuri wa mapenzi haya ya baba yake. Kwa sababu ya mambo ambayo wameifanyia klabu, jina la Muchacho na Simba vitaendelea kudumu, daima na milele," alisema Rage.
MSAJILI.
KLABU ya Simba inapenda kukanusha upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kupitia vyombo vya habari kwamba Katiba ya Simba bado haijapelekwa katika Ofisi za Msajili.
Katiba ya tayari iko kwa Msajili kwa Zaidi ya wiki moja sasa na kilichobaki ni taratibu za kawaida za serikali kuhakikisha kwamba mchakato huu unamalizika kwa faida ya pande zote.
Simba SC inatumia nafasi hii kuwaomba wanachama na wapenzi wake kuwa watulivu wakati wakisubiri Ofisi ya Msajili wa Vyama na Vilabu kufanya kazi yake.
Tangu mwanzo tulikubali kwamba Katiba yetu itatumika mara tu baada ya kupitishwa na TFF na Ofisi ya Msajili ambao wanafanya kila kitu kwa taratibu zao.
Ni vema pia watu wakaacha kueneza maneno ya uongo kuhusu Katiba kutopelekwa kwa Msajili kwa vile taarifa kama hizo zina lengo tu la kupotosha na kutaka kusababisha rabsha hata pasipo na sababu.
Mchezo wa mpira ni wa kistaarabu na ni vema wastaarabu wote wakatulia na kusubiri majibu kutoka katika Ofisi ya Msajili.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Katibu Mkuu
Simba SC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment