STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 18, 2014

Diamond ateuliwa kuwania tuzo 2 MTV

Diamond
NYOTA wa muziki wa Bongofleva, Diamond Platnumz ameendelea kuchana anga la Afrika katika muziki baada ya kutajwa kuwania tuzo mbili za MTV ikiwamo kubwa zaidi ya Msanii Bora wa Kiume Afrika.
Katika majina ya wanaowania tuzo hizo za MTV Africa Music Awards (MAMA) yaliyotangazwa juzi, Diamond anawania tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na pia tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano (Number One remix) alioufanya na Davido wa Nigeria.
Katika tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika, Diamond anachuana na mshirika wake Davido, pamoja na Anselmo Ralph (Angola), Donald (Afrika Kusini) na Wizkid wa Nigeria.
Diamond na Amani wa Kenya wamekuwa wasanii pekee wa kujitegemea kutoka Afrika Mashariki na Kati kuingia kuwania tuzo hizo, wakati Sauti Sol kutoka Kenya wameingia kuwania tuzo ya Kundi Bora Afrika.
Mafikizolo na Uhuru kutoka Afrika Kusini wanaongoza kuwania tuzo nyingi (4) sawa na Davido, ambaye anawania pia wimbo bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Mwaka na Wimbo wa Ushirikiano.
Katika tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano, Diamond na Davido wanachuana na Amani ft Radio & Weasel – ‘Kiboko Changu’ (Kenya/Uganda, Mafikizolo ft May D – ‘Happiness’ (Afrika Kusini/Nigeria), R2bees ft Wizkid – ‘Slow Down’ (Ghana/Nigeria) na
Uhuru ft DJ Buckz, Oskido, Professor, Yuri Da Cunha – ‘Y-tjukutja’ (Afrika Kusini/Angola).
Nyota wa timu ya soka ya Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure anawania tuzo isiyohusiana na muziki ya 'Personality of the Year' akichuana na muigizaji Mkenya aliyeshinda tuzo ya Oscar, Lupita Nyong’o na muigizaji Mnigeria Omotola Jalade
Upigaji wa kura za kuwachagua washindi ulianza Jumatano hadi Juni 4, 2014 usiku kupitia www.mtvbase.com.
Diamond amewashuruku mashabiki wake na kuwaomba wampigie kura ili ailetee heshima Tanzania.

No comments:

Post a Comment