STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 18, 2014

Dominic Nyamisana kuzihukumu Simba, Yanga kesho Taifa

Yanga

Simba
MWAMUZI Dominic Nyamisana kutoka mkoani Dodoma ndiye anayetarajiwa kuchezesha mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga wakati wakifunga msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga itashuka uwanjani ikiwa imeshakata tiketi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika yatakayofanyika mapema mwakani.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Nyamisana atasaidiwa na John Kanyenye kutoka Mbeya na Jesse Erasmo wa Morogoro.
Mbali na klabu hizo kongwe, pia timu nyingine 14 zinazoshiriki ligi hiyo  zitashuka kwenye viwanja tofauti hapa nchini kusaka pointi tatu muhimu.
Mabingwa wapya wa ligi hiyo, Azam ya jijini yenyewe itashuka kwenye Uwanja wa nyumbani Azam Complex kuwakaribisha JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani.
Timu ya Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora tayari imeshashuka daraja huku mchezo kati Ashanti United na Prisons ya Mbeya zitakazocheza mechi yao kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, ukitarajiwa kuamua timu itakayoshuka daraja.
Prisons inahitaji sare yoyote ili kubaki Ligi Kuu, wakati Ashanti ushindi pekee ukiwa ndiyo tiketi yake ya kuonekana tena katika ligi hiyo msimu ujao.

No comments:

Post a Comment