Fernandinho akiifungia City bao la kuongoza dhidi ya Sunderland |
Wachezaji wa Crystal Palace wakishangilia moja ya mabao yao wakati wakiizamisha Everton kwao |
Samir Nasir akiisawazishia Manchester City bao la pili dhidi ya Sunderland |
Everton walipokuwa wakifurukuta kwa Crystal Palace na kuangukia pua usiku huu |
Sunderland wakiandika moja ya mabao yao langoni mw Manchester City usiku huu |
Everton iliyoipisha Arsenal katika nafasi ya nne baada ya The Gunners kupata ushindi mnono jana wa mabao 3-1, ilishuktukizwa na Crystal Palace waliowafuata uwanja wa Godson Park kwa kufungwa bao dakika ya 23 kupitia Jason Puncheon goli lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa wageni kuandikisha bao la pili kupitia kwa Scott Dann dakika nne baada ya kuanza kwa kipindi hicho kabla ya Steven Naismith kuifungia Everton bao la kwanza la kufutia machozi dakika ya 61.
Wageni waliongeza bao la tatu dakika ya 73 kupitia kwa Cameron Jerome kabla ya Kevin Mirallas akaifungia wenyeji bao la pili la kufutia machozi dakika nne kabla ya mchezo huo kuisha.
Kwa matokeo hayo Everton amesaliwa nafasi ya tano na pointi 66, moja zaidi ya ilizonazo Arsenal huku wakiwa wamecheza mechi 33 kila mmoja, Crystal Palace wamechupa hadi nafasi ya 11 wakiwa na pointi 40.
Katika pambano jingine la mfululizo wa ligi hiyo, Manchestwer City ikiwa uwanja wa nyumbani ilishtukizwa na vibonde, Sunderland kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2.
Wenyeji walianza kuandika bao dakika ya pili lililofungwa na Fernandinho akimalizia kazi nzuri ya Kun Aguero.
Hata hivyo Sunderland wanaopigana kuepuka kushuka daraja ilirejesha bao hilo kupitia kwa Cannor Wickham katika dakika ya 73 kabla ya mchezaji huyo huyo kuongeza bao la pili lililowakata maini Manchester City katika harakati za kupunguza pengo la pointi dhidi yake na vinara Liverpool na waliopo nafasi ya pili Chelsea watakaoumana nao hivi karibuni.
Bao hilo la pili Wickham alilifunga katika dakika ya 83 kabla ya Samir Nasir kusawazisha bao hilo dakika mbili kabla ya mchezo huo kumalizika na kuifanya City kuambulia pointi moja na kufikisha 71, nne pungufu na za Chelsea yenye 75 na sita na ilizonazo Livewrpool yenye pointi 77, huku Sunderland ikisalia mkiani na pointi 26.
No comments:
Post a Comment