
Kipigo hicho kimeifanya Roma kusaliwa na pointi 85 na michezo miwili ambapo hata kama wakishinda mechi hizo hawataweza kuzifikia pointi ilizonazo Juve ambazo ni 93 na kuwafanya kibibi cha Turin kuingia uwanja wa nyumbani wakiwa tayari mabingwa wa Seria A.
Katika mechi nyingine za jana nchini humo, AC Milan iliwashikika adabu wapinzani wao wa jiji la Milan, Inter Milan kwa kuwalaza bao 1-0, huku Parma wakishinda nyumbani mabao 2-0 dhidi ya Sampdoria, Udenese ikishinda pia nyumbani mabao 5-3 dhidi ya Livorno, Torino ikiiduwaza Chievo Verona kwa kuwalaza bao 1-0 na Genoa na Bologna zilishindwa kutambiana kwa kutofungana.
No comments:
Post a Comment