STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 14, 2014

Snura abaki njia panda na mbili mpya

NYOTA wa filamu anayekimbiza kwenye muziki, Snura Mushi, amekamilisha nyimbo mbili mpya za 'Ime-expire' na 'Mtaka Basi' japo hajui wimbo gani atakaouachia kati ya hizo.
Nyimbo hizo zimekamilika kurekodiwa chini ya watayarishaji mahiri nchini, Maneke na Adidad na zimekuja baada ya kuachia video ya wimbo wake unaotamba kwa sasa hewani uitwao 'Umeshaharibu'.
Akizungumza na MICHARAZO, Snura maarufu pia kama 'Mama Majanga' alisema atakaa na meneja wake ili kuamua wimbo upi kati ya nyimbo hizo uanze kutoka kwa mashabiki wake.
"Baada ya kuwashushia hewani video ya wimbo wa 'Umeshaharibu', nimekamilisha nyimbo mbili mpya ambazo zijajua upi utakaoanza kuruka hewani kabla ya mwingine kwani zote ni kali," alisema.
Snura alisema kuwa, mara baada ya mojawapo ya nyimbo hizo kuachiwa hewani mchakato wa kutengeneza video zake utaanza mara moja, japo hajajua kazi hiyo itafanyika katika kampuni gani.
"Video zake zitatengenezwa baada ya kuanza kuachiwa hewani kwa moja ya nyimbo hizo," alisema.
Kabla ya 'Umeshaharibu' Snura alitamba na nyimbo za 'Majanja' na 'Umevurugwa' ambazo zimemfanya msanii huyo kuwa matawi ya juu.

No comments:

Post a Comment