STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 14, 2014

Tata kocha mpya wa Argentina kutangazwa rasmi leoALIYEKUWA kocha wa Barcelona, Gerardo 'Tata' Martino amechaguliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Argentina.
Tata amepata ulaji huo baada ya kocha aliyeifikisha fainali ya kombe la dunia Alejandro Sabella kujiuzuru mara tu baada ya kufungwa bao 1-0 na Ujerumani kwenye mchezo wa fainali ya mwaka 2014.
Martino alisitishiwa huduma kwenye klabu ya baada ya kuwa na msimu mbaya huku akiiongoza Barcelona kumaliza msimu bila taji lolote kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.
Martino mwenye umri wa miaka 51 ana uzoefu wa kufundisha soka akiwa ameiongoza timu ya taifa ya Paraguay kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kati ya mwaka 2006 hadi 2011, Martino atatangazwa rasmi leo Alhamis.

Akiwa kocha wa Barcelona aliiongoza timu hiyo kushinda michezo 40 kati ya michezo 59.

No comments:

Post a Comment