STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 21, 2014

Inspekta Harun kuachia mpya akisherehekea miaka 10 ya ndoa yake

Babu akiwa katika pozi tofauti

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Haruna Kahena 'Inspekta Harun' a.k.a Babu anatarajiwa kusherehekea miaka 10 ya ndoa yake kwa kutambulisha wimbo mpya wa 'Hali Bado Tete'.
Wimbo huo alioimba na Luteni Karama ni utambulisho wa ujio mpya wa kundi lililowahi kutamba nchini miaka kadhaa iliyopita ya Gangwe Mob.
Akizungumza na MICHARAZO, Babu alisema sherehe hizo zitakazopambwa na burudani zitafanyika siku ya Jumamosi kwenye ukumbi wa Mpo Afrika, Tandika Davis Corner, jijini Dar es Salaam.
Babu alisema katika sherehe hizo atasindikizwa na wasanii kama TID, Mabaga Fresh, LWP, Scorpion Girls, Dogo Mfaume na wengine na yeye na Luteni Karama watatambulisha wimbo wa 'Hali Bado Tete'.
"Oktoba 25 nitakuwa naadhimisha miaka 10 tangu nifunge ndoa na siku hiyo nitatambulisha kazi zangu mpya ukiwamo wimbo wa 'Hali Bado Tete' unaotangaza ujio wa kundi la Gangwe Mob'," alisema.
Mkongwe huyo alisema mbali na wimbo huo pia atatambulisha nyimbo zake zikiwamo 'Bado Hujachelewa', 'Mungu Ndiye Anayepanga' alioimba na Sir Juma Nature' na nyingine.

No comments:

Post a Comment