STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 21, 2014

Mashetani Wekundu chupuchupu England mechi ya sita bila ushindi ugenini

Daley Blind
Delay Blind akishangilia bao la Fellaine aliyefunmga pia jana
Marouane Fellaini slammed Manchester United level within minutes of coming on as a substitute
Fellaine akishangilia bao la kusawazisha la kwanza la Manchester United
Stephane Sessegnon of West Brom
Stephane Sessegnon akishangilia bao la kuongoza la West Brom
MABINGWA wa zamani wa England, Manchester United usiku wa kuamkia leo wameponea chupuchupu kulala ugenini baada ya kuchomoa bao dakika za lala salama na kuambulia sare ya 2-2 dhidi ya West Bromwich Albion katika pambano la Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Bao lililofungwa dakika tatu kabla ya kumalizika kwa mchezo huo lililofungwa na Daley Blind, liliowaokoa Mashetani Wekundu na kuwapa pointi moja.
Hilo lilikuwa pambano la sita kwa vijana wa Luis Van Gaal kucheza ugenini bila kupata ushindi katika ligi hiyo na kuifanya timu hiyo ishindwe kuingia kwenye Nne Bora tangu ilipoporomoka 'kisoka' msimu uliopita chini ya kocha David Moyes.
Mara ya mwisho Manchester United kukumbana na hali hiyo ya kucheza mechi sita ugenini bila ushindi ilikuwa msimu wa mwaka 1996-1997.
Wenyeji waliandika bao la kuongoza dakika ya nane tu tangu kuanza kwa pambano hilo kupitia Stephane Sessegnon aliyeshindwa kufurukuta mbele ya mabeki wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akiwa na timu yake ya taifa ya Benin iliyolala kwenye uwanja wa Taifa kwa mabao 4-1.
Kiungo mtokea benchi, aliisawazishia Manchester United dakika mbili tangu awe uwanjani katika dakika ya 48 akimalizia pasu nzuri ya Angel di Maria kabla ya Saido Berahino kuiongezea West Brom bao la pili katika dakika ya 66 akimalizia pasi ya Chris Brunt.
Wengi wakiamini Mashetani Wekundu wamelala baada ya kupata ushindi mfululizo katika mechi zake zilizopita, ndipo Blind alipofunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo msimu huu.

No comments:

Post a Comment