STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 21, 2014

Fella athibitisha YP kufariki dunia, mazishi yake yasubiri ndugu

http://3.bp.blogspot.com/_JI2CjMwyBpw/SDBQisbubLI/AAAAAAAACV4/RL3wbYXobbM/s400/YP.jpg
YP enzi za uhai wake

http://www.bongo5.com/wp-content/old/stories/fella_l.jpg
Said Fella
MENEJA wa kundi la TMK Wanaume Family aliye pia mkurugenzi wa MKubwa na Wanae, Said Fella 'Mkubwa' amethibitisha kuwa msanii YP amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Akizungumza na MICHARAZO hivi punde, Fella alisema YP amefariki akiwa katika Hospitali ya Temeke na siyo nyumbani kwao kama taarifa za awali zilizokuwa zimetufikia na kwamba alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kifua.
'Ni kweli YP amefariki akiwa Temeke Hospitali alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa, alikuwa akisumbuliwa na Kifua, kwa kweli ni pigo kwetu na tasnia nzima ya muziki kwani ni hivi karibuni tumetoka kumpoteza pia Side Mnyamwezi," alisema Fella mmoja wa wadu wa muziki waliosaidia kukuza muziki wa kizazi kipya kwa kuibua vipaji kila uchao. 
Fella alisema kwa sasa wanasubiri kuwasiliana na ndugu na familia ya marehemu YP kwa ajili ya kujua mazishi yake yatafanyika lini na wapi, japo alisema huenda atazikwa kesho pande za TMK.
Enzi za uhai wake YP alitamba na wimbo wake mkali wa 'Binadamu Visa' alioimba na swahiba wake, Y Dash na pia alishiriki kwenye wimbo wa Dar Mpaka Moro na wasanii wenzake wa TMK, Chegge na Mheshimiwa Temba.
Nyimbo nyingine alizowahi kuimba ni 'Ulipenda Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' akiwa na Y Dash pia alitamba na 'Twende Zetu' ya Chege,  'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.

No comments:

Post a Comment