STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, November 5, 2014

HIZI NDIZO ZA KWANZA KUFUZU 16 ULAYA

Karim Benzema scores Real Madrid's opener against LiverpoolAleksander Mitrovic scores a dramatic last minute equaliser for Anderlecht against ArsenalBorussia DortmundWAKATI kivumbi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ikitarajiwa kuendelea usiki wa leo, michuano hiyo jana ilishuhudia timu mbili za Real Madrid ya Hispania na Borussia Dortmund ya Ujerumani zikiwa timu za kwanza kufuzu hatua ya 16 Bora katika makundi yao.
Madrid aliwapata nafasi hiyo baada ya kuidonyoa Liverpool kwa bao 1-0 lililofungwa na Karim Benzema, katika mechi za Kundi B, wakati Dortmund inayonolewa na Jurgen Klopp iliinyuka Galatasaray kwa mabao 4-1 n kufuzu hatua hiyo kutoka kundi D.
Timu zimefikisha jumla ya pointi 12 kila moja katika kundi lake na kufuzu moja kwa moja katiak hatua inayofuata na kusubiria kujua timu itakazoungana nazo kwenye mechi za raundi ya tano zitakazochezwa baadaye.
FC Basel wapo nyuma ya Real Madrid baada ya usiku wa jana kuinyuka Ludogorets Razgrad ya Bulgaria kwa mabao 4-0.
Mabingwa wa La Liga, Atletico Madrid ilitakata ugenini baada ya kuilaza Malmo kwa mabao 2-0 katika mechi ya kundi A huku Olympiakos wakisalia nafasi ya pili baada ya kunyukwa ugenini mabao 3-2 na Juventus.
Katika mechi za Kundi C Bayer Leverkusen wamejiimarisha kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya Zenit Saint Petersburg, Benfica wao walifufua matumaini yao ya kusonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Monaco.
Arsenal wao wameendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Dortmund baada ya kushindwa kulinda ushindi wake na kujikuta wakitoa sare ya mabao 3-3 na Anderletch katika Uwanja wa Emirates.
Timu hiyo ilikuwa mbele kwa mabao 3-3 hadi dakika ya 60 kabla ya wageni kurudisha bao moja baada ya jingine na kufanya matokea kuwa sare na kumkasirisha meneja wao Arsene Wenger aliyeitupia lawama safu yake ya ulinzi.

Copy n Win at: http://bit.ly/copy_win

No comments:

Post a Comment