STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 10, 2014

Arsenal yaua, Monaco Juve zapenya 16 Bora Ulaya

Wojciech Szczesny (left) looks on in shock as Arsenal players celebrate Ramsey's stunning strike
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia bao lao kwa kumfuta kiatu Aaron Ramsey
Lukas Podolski fires past Galatasaray defender Semih Kaya to give Arsenal an early lead in the Group D clash
Podolski akifunga bao la kwanza la Arsenal
sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid ilitosha kuwavusha Juventus kwenye hatua ya 16 bora.
Wachezaji wa Juventus walifurahia baada ya timu yao kufuzu hatua ya 16 Bora
The Juventus squad couldn't hide their delight at progressing to the knockout stages of the Champions League on Tuesday evening
Hureeee!
Monaco nao walikuwa na furaha yao kama hivi

Bayer Leverkusen went through, but were disappointed at full-time after surrendering top spot to Monaco
Bayer Leverkusen naop wamefuzu 16 Bora
MABAO mawili ya kila mmoja toka kwa Aaron Ramsey na Lucas Podolski yaliiwezesha Arsenal ya Uingereza kupata ushindi mnono ugenini wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji wao Galatasaray ya Uturuki na kujihakikishia nafasi ya pili katika Kundi D la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Podolski aliiandikia The Gunners bao la kuongoza dakika ya tatu tu tangu kuanza kwa pambano hilo kabla ya Ramsey kuongeza la pili dakika ya 11 na kisha kurudi tena kambani dakika ya 29.
Kipindi cha pili wenyeji walicharuka na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na mkongwe Wesley Sneijder kwa mpira wa adhabu ndogo katika dakika ya 87.
Dakika tatu baadaye Ramsey alihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne na la pili kwake katika mchezo huo na kuifanya Arsenal ikitinga hatua ya 16 Bora nyuma ya Borussia Dortmund ya Ujerumani ambayo ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Anderlecht ya Ubelgiji.
Vijana hao wa Arsene Wenger wana hatari ya kukutana na moja ya timu mojawapo kati ya Real Madrid, Atletico Madrid, Barcelona, PSG, Bayern Munich, Porto au Monaco katika hatua ya mtoano.
Bao la Dortmund lilifungwa na Ciro Immobile katika dakika ya 58 kabla ya wageni kuchomoa dakika sita kabla ya kumalizika kwa pambano hilo kupitia kwa Aleksandar Mitrovic  kwa njia ya kichwa.
Dortmund imeongoza kundi hilo kwa sare hiyo kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, lixcha ya kulinga pointi 13 na Arsenal.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Juventus ikiwa nyumbani ililazmisha suluhu kwa Atletico Madrid na zote mbili kufuzu kwa hatua ya 16 Bora kutoka kundi A, licha ya Olympiakos Pirates kupata ushindi mnono wa mabao 4-2 djhidi ya Malmo ya Sweden.
Nayo timu ya Monaco ya Ufaransa ilifanikiwa kusonga mbele baada ya kuilaza Zenit St Petersburg ya Russia kwa mabao 2-0 na kuongoza kundi C ambalo lilishuhudia Bayer Leverkusen wakifuzu nao licha ya kung'ang'aniwa ugenini na Benfica ya Ureno.

ZILIFUZU 16 BORA
Kundi A: Atletico Madrid na Juventus
Kundi B: Real Madrid na Basle
Kundi C:Monaco na Bayer Leverkusen
Kundi D: Borussia Dortmund na Arsenal

No comments:

Post a Comment