STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 10, 2014

Liverpool yakwama, Real Madrid yaua Ulaya

Steven Gerrard looks forlorn after the final whistle as Liverpool are knocked out of the Champions League by Basle
Nahodha Steven Gerrard haamini kilichoikuta timu yake jana usiku
Basle players celebrate their qualification to the Champions League knockout phases as Bjorn Kuipers blows the final whistle
Basle wakishangilia bao lao lililofungwa na Frei
Croatian defender Dejan Lovren protests as substitute Markovic is shown a straight red card for catching Safari
Nenda nje sitaki uhuni uwanjani
Ronaldo celebrates with Gareth Bale and Javier Hernandez after scoring from the spot against Ludogorets
Ronaldo akipongezwa na wenzake
Medran scored his first Champions League goal for Real Madrid after coming off the bench for the last seven minutes
Medran akifunga bao la nne la Real Madrid
KLABU ya Liverpool imekwama kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na timu ya Basle, wakati Real Madrid ikipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Ludogorets katika mechi za Kundi B.
Ushindi huo umeiwezesha Real madrid kuongoza kundi hilo, wakati Liverpool iliyokuwa ikihitaji ushindi ili kusonga mbele imeishia kukamata nafasi ya tatu nyuma ya Basle ambayo sasa inaungana na Real madrid kusonga mbele baada ya sare ya ugenini.
Liverpool wakiwa kwenye uwanja wao wa Anfield walishshtukizwa na wageni wao kwa kufungwa bao katika dakika ya 25 kupitia Fabian Frei na kulazimika kulichomoa katika kipindi cha pili baada ya Lazar Markovic kufunga katika dakika ya 60 na kuongoza msimamo wa kundi B.
Katika pambao jingine la kundi hilo la B, Real Madrid wakiwa nyumbani waliishindilia Lodogorets kwa mabao 4-0, huku Cristiano Ronaldo akifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Marelonho wa Logorotes kucheza rafu iliyomfanya atolewe nje kwa kadi nyekundu na kumfanya nyota huyo kumfikia gwiji wa zamani wa klabu hiyo Raul Gonzalez kwa idadi ya mabao aliyofunga kwenye michuano hiyo.
Ronaldo alifunga bao hilo katika dakika ya 20 na kumfanya kufikisha jumla ya mabao 72 na kusaliwa mabao mawili kumfikia hasimu wake, Lionel Messi mwenye mabao 74, ambaye usiku wa leo atakuwa dimbani tena kuiwakilisha Barcelona dhidi ya timu ya PSG.
Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa naGareth Bale katika dakika ya 38 kabla ya weatokea benchi Alvaro Arbeloa na Alvaro Medran kufunga mabao mengine katika dakika za 80 na 88.

No comments:

Post a Comment