STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 21, 2015

Ronaldo adaiwa kujituliza kwa Mtangazaji wa runinga

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo aliyetangaza kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu mwanamitindo , Irina Shayk, amedaiwa kuangukia mikononi mwa kimwana mpya Mtangazaji wa kituo cha Televisheni chaHispania, Lucia Villalon.
Kwa mujibu vyanzo vya habari vya karibuni na mwanasoka huyo vinasema kuwa Mreno huyo aliyetoka kunyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia (FIFA Ballon 'dOr) kwa mara ya pili mfululizo na tuzo ya tatu kwake kwa sasa anatoka na mtangazaji huyo.
Picha iliyomuonyesha Ronaldo akiwa na kimwana huyo wakipongezana mara baada ya nyota huyo kufanikiwa kunyakua tuzo hiyo ya Ballon d'Or akiwashinda Lionel Messi na Manuel Neuer, imedaiwa ndiyo chanzo cha hisia hizo kwamba huenda mtangazaji huyo ndiyo aliyeziba nafasi ya Irina, ambaye hakuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika nchini Uswisi.
Ronaldo alifichua juu ya tetesi ya kumwagana na Irina, aliyemudu naye katika mahusiano kwa miaka mitano na kueleza alikuwa anapaswa aache kuendelea na mambo yake baada ya tukio hilo la kumwagana na mwanamitindo huyo.
Hata hivyo vyombo vya habari vimedokeza, Ronaldo na Villalon wanatoka pamoja na ndiyo maana kimwana huyo mwishoni mwa wiki alitupia kwenye akaunti yake ya twitter ujumbe kuonyesha alikuwa akifuatilia pambano baina ya Getafe na Real Madrid lililoisha kwa Madrid kushinda mabao 3-0, mawili kati ya hayo yakifungwa na Ronaldo na jingine likitumbukizwa wavuni na Gareth Bale.

No comments:

Post a Comment