STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 21, 2015

Kocha Aston Villa asisitiza Benteke haendi kokote

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2012/11/27/article-2239412-163DB1CE000005DC-38_634x375.jpgMENEJA wa klabu ya Aston Villa, Paul Lambert amesema mshambuliaji wao nyota, Christian Benteke haondoki klabu hapo, hata kama kuna tatizo la ufungaji katika kikosi chake.
Klabu ya Villa ndfiyo timu yenye idadi ndogo ya magoli katika Ligi Kuu ya England na imekuwa ikidaiwa kuwa huenda ikaachana na Benteke ili kusajili mchezaji mwingine mkali wa kutatua tatizo jilo la ufungaji.
Hata hivyo, Lambert amesema kuwa hakuna mahali kokote mshambuliaji huyo atakapokwenda licha ya kikosi chake kushika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi pointi tatu juu ya eneo la hatari ya kushuka daraja.
Kikosi hicho cha Villa hakijafunga bao lolote katika mechi tano zilizopita za karibuni ikiwa na mabao 11 katika mechi 22 walizocheza, lakini Lambert amesema bado wanamhitaji Benteke.
Pia kocha huyo alimsifia Benteke akisema kuwa ni mmoja wa washambuliaji bora barani Ulaya na kwamba klabu yao haiwezi kumuacha kirahisi licha ya kasi yake ya kufumania nyavu kupungua baada ya kutoka kwenye majeraha.
Mshambuliaji huyo kutokla Ubelgiji, amefunga mabao mawili tu msimu huu katika mechi 13 alizoichezea timu yake na amekuwa akidaiwa kunyemelewa na baadhi ya klabu katika dirisha la usajili linaloendelea.

No comments:

Post a Comment