STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 2, 2015

Chegge, Mhe Temba, Madee kuzindua video zao Escape One

http://2.bp.blogspot.com/-Vu_5gWGZci0/VLTBwh0uQjI/AAAAAAAAHGU/dde5fCkSruY/s1600/Madee%2B-%2BVuvula.jpgWASANII nyota nchini Mhe Temba, Chegge na Madee wanatarajiwa kuzindua rasmi video ya nyimbo zao mpya walizorekodiwa nchini Afrika Kusini wakimshirikisha Dj Maphorisa wa Uhuru.
Meneja wa wasanii hao, Said Fella aliliambia MICHARAZO kuwa, uzinduzi wa video hizo utafanyika siku ya Jumamosi  kwenye ukumbi wa Escape One, Mikocheni.
Fella alisema Madee atazindua video ya wimbo wake uitwao 'Vuvula' wakati Chegge na Mhe Temba watazindua 'Kaunyaka' ambazo zinafanya vema kwenye vituo vya radio na televisheni.
Meneja huyo alisema uzinduzi huo utapambwa na burudani za wasanii kadhaa nyota watakaousindikiza akiwataja baadhi kuwa ni Diamond, Yamoto Band, Jux, Vanessa Mdee, Shaa na wengine.
"Madee, Chegge na Mheshimiwa Temba wanatarajia kuzindua video za nyimbo zao zinazoendelea kutamba hewani kwa sasa, uzinduzi utafanyika Escape One na utasindikizwa na wasanii kadhaa nyota akiwamo Diamond, Shaa, Vee Money na wengine," alisema Fella.

No comments:

Post a Comment