STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 2, 2015

Newz Alert! Francis Cheka ahukumiwa miaka mi3 jela

Cheka (kulia) katika mikutano ya mapambano yake pembeni yake ni promota Omar Kimbau
BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa nchini aliyewahi kuwa Bingwa wa Dunia wa WBF, Francis Cheka 'SMG' mwenye maskani yake mjini Morogoro amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.
Kwa mujibu wa kituo cha redio cha EFM kipindi cha Sports Headquarter, Cheka amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga meneja wake katika shughuli zake za biashara ya ukumbi wa Vijana Social mjini Morogoro anayedaiwa kumuingiza mjini kiasi kikubwa cha fedha kiasi cha kufikia kuchapana naye.
Akizungumza na kituo hicho baba mzazi wa Francis Cheka amesema haikuwa sahihi kwa mwanae kupewa hukumu hiyo na badala yake wangekaa na kuzungumza ili kuyamaliza matatizo hayo.
Mzee huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kuna watu wenye chuki na mwanae wameitumia kesi hiyo ya muda mrefu kutimiza malengo yao lakini pia mzee huyo ameelezea hisia zake kwa wakazi wa Morogoro kutoa sapoti ndogo kwa mwanae.
Taarifa zinasema kuwa Cheka amehukumiwa adhabu hiyo leo JUmatatu Februari 2, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
EFM.

No comments:

Post a Comment