STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 2, 2015

Shaa kutoa mpya, video ya Subira bado yakwama

WAKATI video ya wimbo wake wa 'Subira' ikiwa inaendelea kupigwa danadana bila kuachiwa tangu itengenezwe, msanii Sarah Kais 'Shaa' yupo njiani kuachia kazi mpya.
Akizungumza na MICHARAZO mapema leo, Meneja wa msanii huyo Said Fella 'Mkubwa' alisema kuwa katikati ya mwezi huu Shaa ataachia kazi mpya kulingana na utaratibu waliojiwekea.
Akiwa chini ya Mkubwa na Wanae, Shaa ameshaachia nyimbo mbili za 'Sugua Gaga' na 'Subira' na hivi karibuni akiwa Kenya kikazi alitoa wimbo mpya uitwao 'Njoo' akishirikiana na mkenya Redsan.
"Tupo katika maandalizi ya mwisho kabla ya Shaa kuingia studio kutengeneza kazi mpya," alisema Fella na kufafanua juu ya video ya wimbo wa 'Subira' ambao ina muda mrefu tangu itangazwe itaachiwa hadharani bila mafanikio.
"Video hiyo imeshakamilika kitambo ila bado ipo mikononi mwa Adam Juma aliyeitengeneza, tukikabidhiwa tutaiachia mara moja," alisema Fella.
Alipoulizwa sababu ya kucheleweshwa kwa video hiyo alisema kuna mambo ambayo hawajaridhishana katika video hiyo ya 'Subira' ambayo ilitengenezwa mwishoni mwa mwaka jana kabla ya Shaa hajaenda Kenya.

No comments:

Post a Comment