STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 11, 2015

Mourinho amchongea Van Persie kwa FA

MENEJA wa vinara wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekishambulia Chama cha Soka cha Uingereza(FA) kwa kuamua kutochukua hatua yeyote kwa mshambuliaji wa Manchester United, Robin Van Persie kwa tuhuma za kumtwanga kiwiko mchezaji wa upinzani.
Van Persie alionekana akimpiga kiwiko James Tomkins wakati wa mchezo ambao United ilitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya West Ham United Jumapili iliyopita lakini mwamuzi Mark Clattenburg hakuona tukio hilo huku FA nao wakilifumbia macho.
Uamuzi huo unamfanya Mourinho kutowaelewa FA kwani anatarajiwa kumkosa nyota wake Diego Costa katika mchezo wa leo dhidi ya Everton baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania kufungiwa mechi tatu kwa kukutwa na hatia ya kumkanyaga kwa makusudi Emre Can mwezi uliopita.
Akihojiwa Mourinho amesema watu haohao ambao wamemfungia mchezaji wake Costa ndio hao ambao hawataki kumfungia Van Persie kwa kosa lake alilofanya.
Mourinho aliendelea kudai kuwa anajua kama angekuwa mchezaji wake lazima angefungiwa kwani tukio kama hilo lilimtokea Ramires na alilimwa adhabu.

No comments:

Post a Comment