STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 11, 2015

Sanchez, Ramsey wazua hofu Arsenal

http://www3.pictures.zimbio.com/gi/Aaron+Ramsey+Alexis+Sanchez+Leicester+City+N8Hb6G9P6Rgl.jpg
Ramsey, SanchezKOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ana wasiwasi kuhusu hali za nyota wake Alex Sanchez na Aaron Ramsey baada ya kupata majeruhi katika mchezo Ligi Kuu walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Leicester City.
Ramsey alitolewa nje ikiwa ni dakika tisa tu toka aingie akitokea benchi katika kipindi cha pili baada ya kupata majeruhi ya msuli wa paja, huku winga wa kimataifa wa Chile, Sanchez yeye alitolewa nje kufuatia kuchezewa faulo na Matthew Upson ambayo ilimfanya kushindwa kuendelea na mchezo huo uliochezwa Emirates.
Wenger amesema ana wasiwasi na nyota wake hao kwani hana uhakika watakaa nje ya uwanja kwa kipindi gani wakijiuguza. Mabao yaliyofungwa na Laurent Koscielny na Theo Walcott yalitosha kuwapa Arsenal ushindi huo muhimu baada ya kuchapwa na  Tottenham Hospur
Mabao yaliyofungwa na Laurent Koscielny na Theo Walcott yalitosha kuwapa Arsenal ushindi huo muhimu baada ya kuchapwa na mahasimu wao Tottenham Hotspurs mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment