STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 11, 2015

Azam yaifumua Mtibwa Sugar 5-2 warudi kileleni

KLABU ya Azam wamerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifumua bila huruma Mtibwa Sugar kwa mabao 5-2.
Azam ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wealipata ushindi huo mnono na wa kwanza kushuhudiwa katika mechi za ligi msimu huu katika pambano pekee lililochezwa kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Frank Domayo 'Chumvi' alifunga mabao mawili moja kila kipindi sawa na alivyofanya Kipre Tchetche na Didier Kavumbagu alifunga moja kuiangamiza Mtibwa ambao hicho ni kipigo chao cha pili mfululizo.
Mtibwa walioanza msimu huu kwa mkwara na kuongoza ligi hiyo kwa muda mrefu kabla ya kuporomoka mara baada ya kurejea kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ilifunikwa eneo la kiungo na Azam.
Vijana hao wa Mecky Mexime walipata mabao yao ya kufutia machozi kupitia kwa Juma Nampaka na Ame Ali ambayo hata hivyo hayakusaidia Wakata Miwa hao kufurukuta mbele ya mabingwa watetezi hao.
Kwa ushindi huo umeifanya Azam kurejea tena kileleni wakifungana pointi 25 sawa na Yanga, lakini tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa yanawapa nafasi ya kukalia kiti cha uongozi.
Mtibwa wenyewe wameendelea kusalia katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 18 sawa na ilizonazo timu za Kagera Sugar na Coastal Union.
Yanga na Azam zinazochuana kieleleni mwishoni mwa wiki zitakuwa kwenye majukumu ya kimataifa wakati Yanga itaikaribisha BDF XI ya Bostwana na wenzao Azam wataumana na El Merreikh wanaotarajiwa kutua nchini kesho tayari kwa pambano hilo litakalochezwa Jumapili.
Pambano la Yanga litacheza Jumamosi na viingilio vimeshjatangazwa kwa kiingilio cha chini kikiwa ni Sh 5000 tu.
Wakati lile la Yanga kiingilio cha chini kabisa ni Sh 2000 na vingine ni VIPB Sh 5000 na VIP A 10000 na tyiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa.

No comments:

Post a Comment