STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 17, 2015

Boateng kurejea tena San Siro

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/06/26/article-2670725-1F2594FC00000578-295_634x645.jpgTENA? Aah haiwezekani! Wakala wa Kevin-Prince Boateng amethibitisha kuwa kiungo huyo anaweza kujiunga tena na AC Milan katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ghana alikaa San Siro kwa miaka mitatu na kufanikiwa kushinda taji la Serie A katika msimu wake wa kwanza kabla ya kuondoka kwenda Schalke ya Ujerumani Agosti mwaka 2013. 
Hata hivyo, Boateng anataka kuondoka Schalke baada ya kusimamishwa na klabu hiyo Mei 11 mwaka huu kufuatia kichapo walichopata dhidi ya Koln. 
Wakala wa Boateng, Federico Pastorello amesema kwa sasa wanasubiri ofa, lakini akakiri kuwa uwezekano wa kurejea Milan ni mkubwa. 
Milan baada ya kumtimua kocha Filippo Inzaghi 'Pippo' na kumuajiri Sinisa Mihajlovic, inategemewa kutenga fungu kubwa kwa ajili ya usajili kiangazi hiki ili kurejesha makali yao baada ya kumaliza msimu wa Serie wakiwa nafasi ya 10.

No comments:

Post a Comment