STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 21, 2015

Utukutu wamponza Neymar, afungiwa mechi nne Copa America

Mshikemshike baada ya Neymar kuzua tafran kwa kupiga mpira ulio 'mbabua' mgongoni mchezaji wa Colombia
Neymar (10) akizozana na wachezaji wa Colombia huku akizuiwa na wenzake wa Brazil
Neymar vurugu
Kwani we unataka nini? Neymar akizozana na wachezaji wa Colombia huku mwamuzi akiteta naye
AMA kweli hasira hasara! Straika tegemeo na nahodha wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr anatarajiwa kuikosa michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile baada ya kufungiwa kucheza mechi nne. 
Mshambuliaji huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 23 alionyeshwa kadi nyekundu kwa kuzozana na wachezaji wa Colombia kufuatia kipigo cha bao bao 1-0 walichopata Brazil katika mchezo wao wa makundi. Mbali na kadi ya moja kwa moja, lakini inadaiwa kuwa Neymar alimtolea lugha ya matusi mwamuzi wa pambano hilo na ndiyo sababu ya kuadhibiwa kukosa mechi nyingine za ziada badala ya moja tu ya kadi aliyopewa.
Nyota huyo tayari anatumikia adhabu ya kutocheza mechi moja hivyo kumfanya kutokuwepo katika mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Venezuela utakaochezwa usiku wa leo.
Lakini Shirikisho la Soka la Amerika Kusini sasa limepitia tukio hilo na kuongeza adhabu kwa nyota huyo baada ya kudaiwa ripoti ya mwamuzi ilitaarifa kumtusi. 
Mchezaji wa Colombia Carlos Bacca ambaye pia alipewa kadi nyekundu katika tukio hilo naye amepewa adhabu ya kutocheza mechi mbili huku wachezaji wote wakipewa nafasi ya kukata rufani kama hawakuridhika na adhabu.

No comments:

Post a Comment