STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 24, 2016

Mbeya City yaibomoa Prisons, yamnyakua mfungaji wao mkali

IMG_20160623_220042
Mkopi akisaini mkataba wa kuichezea Mbeya City
MSHAMBULIAJI nyota wa kikosi cha Prisons-Mbeya, Mohammed Mkopi ameikacha timu hiyo na kutua Mbeya City FC.
Mkopi aliyesaidia na Jeremiah Juma kuibeba Prisons katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita wakifunga jumla ya mabao 21 amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.
Mara baada ya kusaini kandarasi hiyo, Mkopi, aliyewahi kucheza pia timu ya Mtibwa Sugar alisema  kuwa anamshukuru Mungu kwa kufanikiwa kujiunga na City timu ambayo alikuwa na ndoto za kuichezea  hata kabla ya kusajiliwa na Prison msimu uliopita.
“Kabla sijasajiliwa na Prisons ndoto yangu ilikuwa ni kucheza kwenye timu hii, nashukuru Mungu baada ya msimu mmoja hili limefanikiwa, nitakuwa hapa msimu ujao, lengo langu ni kufanya kazi kwa nguvu  ili niendelee kuwa sehemu ya kikosi hiki kwa muda mrefu zaidi” alisema aliyefunga mabao matano msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment