STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 24, 2016

Southampton yampotezea Pellegrini, njia nyeupe kwa Puel

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2016/06/nintchdbpict000233254556.jpg?w=688
Manuel Pellegrini
http://i.eurosport.com/2016/02/06/1790003-37797351-2560-1440.jpg?w=1050
Claude Puel
http://e0.365dm.com/16/06/768x432/victor-wanyama-spurs_3489343.jpg?20160623221243
Victor Wanyama aliyetua Spurs
IKIWA imeshampoteza kiungo mkabaji wake, Mkenya Victor Wanyama, klabu ya Southampton imedaiwa kuachana na mpango kumnyakua kocha wa zamani wa Manchester City, Manuel Pellegrini.
Klabu hiyo ilidaiwa ilikuwa mbioni kumpa ajira Kocha Pellegrini mwenye miaka 62 ili kuziba nafasi ya Ronald Koeman aliyetimkia Everton, hata hivyo mpango huo umefutwa na sasa inaelezwa njia nyeupe kwa Mfaransa, Claude Puel wa klabu ya Nice.
Imeelezwa Southampton imeachana na Pellegrini na kumgeukia Puel anayeinoa Nice kutokana na kubaini katika mazungumzo yao Kocha huyo kutoka Chile hawezi kuendana na falsafa ya klabu hiyo katika suala zima la maendeleo ya soka la vijana.
Mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa na shauku kubwa ya kumuona bosi huyo wa zamani wa Real Madrid na Villareal, aliyetwaa taji la Ligi Kuu ya England miaka miwili iliyopita akitua klabu kwao ili kuchukua nafasi ya Kocha Ronald Koeman aliyewakacha na kuhamia Everton mapema mwezi huu kwa ajili ya msimu ujao.
Southampton inahaha kusaka kocha wakati kiungo wake Mkenya Victor Wanyama akiwa ametimka zake Tottenham Hotspur aliposaini mkataba wa miaka mitano kwa ajili ya msimu ujao na kumpa nyota huyo fursa ya kukipiga Ligi ya Mabingwa Ulaya
.

No comments:

Post a Comment