STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 24, 2016

Yanga yakwama kotekote dhidi ya Tp Mazembe


Kikosi cha Yanga

Mashabiki wa Yanga
WAMEKWAMA kotekote. Klabu ya Yanga ilipanga mechi yao dhidi ya TP Mazembe ichezwe usiku wa Jumatano, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likaigomea. Haikuchoka ikatafuta mbinu nyingine na kuzuia kigoma cha Wakongo kinachoshangilia bila kuchoka wakiungane na watani zao, Simba kwenye Uwanja wa Taifa kwa kutaka kuhodhi majukwaa yote, nalo likagonga mwamba mbele ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyowagomea leo Ijumaa.
TFF kupitia Afisa Habari wake, Alfred Lucas imesema Yanga hairuhusiwi kuyakalia majukwaa yote kama walivyoomba na wakidhubutu wataipata freshi, kwani Kamati ya Mashindano imegomea mchongo wao huo.
Akizungumza leo, Lucas alisema mpango huo wa Yanga hakubaliki na kwamba watatumia jukwaa lao na mengine watatumia wapinzani na watu wengine watakaofika uwanjani Jumanne ijayo, siku itakayopigwa mechi hiyo.
Mechi hiyo itapigwa Saa 10 jioni ya Juni 28 na sio Saa 1:30 usiku wa Jumatano kama walivyoomba awali Yanga kwa sababu wamechelewa kuwasilisja ombi hilo ofisi za CAF ambazo zimewajibu kuwa ratiba itakuwa ile ile ya awali ya Juni 28.
Yanga inahitaji ushindi kwenye mchezo huo wa pili kwao na wa kwanza nyumbani katika Kundi A ya michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kulala ugenini 1-0 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.
Mazembe wanatarajia kutua nchini Jumapili wakipishana saa chache tu na Yanga ambao kwa sasa wapo kambini Antalya wakijifua kujiandaa na mchezo huo.
Baada ya mechi hiyo Yanga inayonolewa na Kocha Hans Pluijm itawasubiri Waghana wa Medeama kwa mchezo wao mwingine katikati ya Julai kabla ya kuifuata kwao Ghana, ambapo ni lazima ishinde mechi hizo tatu kufufua tumaini ya kutinga nusu fainali ili waogelee mihela ya CAF kupitia michuano hiyo ya pili kwa ukubwa Afrika kwa ngazi za klabu baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Msimamo wa Kundi A:

Mazembe  1 1 0 0 3 1 3
Bejaia       1 1 0 0 1 0 3
Yanga       1 0 0 1 0 1 0
Medeama  1 0 0 1 1 3 0 

No comments:

Post a Comment