STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 23, 2016

RB Battery yanogewa Mbeya City, yaongeza mkataba mpya

KAMPUNI ya BinSlum Tyre ya jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi imesaini mkataba mpya wa miaka miwili wenye thamani ya Sh. 360 Milioni kuendelea kuidhamini klabu ya Mbeya City FC.
777
Mara baada ya kusaini mkataba huo, Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohammed BinSlum alisema, licha ya City kuwa na matokeo yasiyoridhishwa kwa msimu uliopita, lakini wameridhishwa kwa kiasi kikubwa namna ambavyo timu hii ilishiriki katika kuitangaza bidhaa yao  na kuifikisha sehemu ilipostahili kufika.
“City haikuwa na matokeo mazuri msimu ulipopita, lakini hatuna shaka na namna walivyoitangaza bidhaa yetu, imani yetu kubwa ni kuwa  mkataba huu mpya itakuwa chachu kwao ya kufanya vizuri zaidi msimu ujao,”  alisema BinSlum.
Naye Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwasilindi, aliishukuru kampuni ya BinSlum kwa kuthamini mchango wa City licha ya matokeo mabaya  msimu uliopita ambapo timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya nane.
“Hatukuwa sawa msimu uliopita, matokeo tuliyoyapata si yale ambayo tumekuwa tukiyapata misimu miwili iliyopita, imani yangu kubwa tutafanya vizuri msimu ujao, nawashukuru BinSlum kwa kutambua mchango wetu kwao, hii ni chachu kwetu kuelekea mafanikio ya msimu ujao” alisema.
ccc

No comments:

Post a Comment